Adsense application sehemu 01


Najua kila mtu akifikia uamuzi wa kufungua blog au website lazima awe na malengo fulani na kikubwa zaidi huwa anafikilia baadae imlipe hiyo website/blog. kitu cha kwanza huwa wanaangalia jinsi gani anaweza kujiunga na adsense na akakubaliwa ili aweze kuingiza pesa. mara nyingi blog nyingi za kitanzania zinakataliwa kutokana na kutokuelewa vizuri vigezo vya kujiunga na hili campany kubwa duniani.

ADSENSE NI NINI?
Adsense ni campany ambalo linajiuhhusisha na kushapisha matangazo na kuyatangaza kwenye blog na website duniani. Ni campany linalomilikiwa na google ndio maana kwenye blogspot wameweka ta yao ya kujiunga moja kwa moja.Ni campany ambalo linalipa vizuri na halina longolongo katika kulipa.

HATUA  ZA KUFUATA ILI KUHAKIKISHA WANAKUKUBALIA KUWEKA MATANGAZO YAO KATIKA BLOG/WEBSITE YAKO.
  • KUTAMBUA VITU WANAVOVIITAJI NA AMBAVYO HAWAITAJI
  • KUFANYA APLICATION
  • KUWEKA ADS CODE KWENYE WEBSITE YAKO
  • KUFUATA SHERIA ZAO ILI KUHAKIKISHA HAWAKUZUII
  • KUFANYA APPLICATION YA PESA

TAMBUA ADSENSE TERMS AND POLICY 

Ndugu msomaji wa makala hii najua unajiuliza kwa nini nimeanza na hili? Kwa sababu nahitaji tujue campany linataka nini na halitaki nini ili unapoiangalia website yako unajua kuwa imekidhi vigezo aua laa.
  1. TERMS AND POLICY KABLA HUJAJIUNGA(Technical requirements)

Kutokana na google kuwa ni kampuni bora kwa advertiser na kuwathamini pia limeweka sheria zifuatazo ambazo website yoyote lazima ifuate ili waikubalie.
  • Use supported languages
Ndugu msomaji inatakiwa website yako itumie lugha ambazo adsense wameziruhusu ili kuweka matangazo yao hadi sasa bofya hapa kuona lugha hizo adsense supported language 
  • Prohibited content
Ndugu msomaji wa makala hii inatakiwa website yako isihusike na vitu vifuatavyo 
  1. adult content( pornography), 
  2. website inayochochea ugomvi (politics), 
  3. website inayohusu madawa ya kulevya,
  4.  Website inayohusu pombe na sigara
  5. Website inayohusiana afya-inayouza dawa zisizo thibitishwa,kutoa ushauri wa kupotosha, kuuza dawa online
  6. Hacking and cracking content - Haitakiwi kuhusika na kucrack na kuhack any thing so haziluhusiwi website za namna hyo
  7. Pages that offer compensation programs-Hitakiwi website yako iwe inatoa ahadi kwa malipo atakayetembelea,atakaye bofya ads hizo hazitakiwi kabisa
  8. Kushawishi kwa matangazo ya uongo- Hizi website haziruhusiwi kabisa inatakiwa kuwa mkweli na mwaminifu katika website yako
  9. Picha za kutisha kama kuvunjika mfupa,ajali mbaya,nguo za kubana,fupi,picha za kupigana,groly video kwa hiyo wanaruhusu boxing na martial arts page tuu
  10. Website ambayo inahusika na silaha kama visu,bomb,bunduki haziruhusiwi
  11. Website ambayo inahusika na kugushi document mbalimbali kama vitambulisho,vyeti
  12. Website ambayo inahusika na vitu ambavyo sio halali kama kuuza bidhaa ambayo inatrade mark ya mwingine,maswala ya sex arts hizi website haziruhusiwi kujiunga
  • Copied Images
Google hawatakukubalia kama website yako inaimage ambazo umecopy kutoka google search, kwa hiyo wanaitaji picha halisi ulizopiga wewe mwenyewe.
  • Too much Ad networks 
Kabla kujiunga hakikisha unaondoa ads zote za makampuni  mengine ndipo ujiunge, Hii ni kwa sababu wanaogopa kuwa hata wakikubalia ads zao hazitaonekana kutokana na kuwa ads nyingi.
  • Sufficient Content
Website yako inatakiwa kuwa na post kuanzia kumi ulizoziandika mwenyewe na ziwe ndefu zisizokuwa na picha nyingi. Na avoid kucopy post nyingine na kuweka kwako inatakiwa uandike hizo posti ndipo wanaweza kukuballia
  • Domain Type and Age
Website yako inatakiwa iwe na domain ya kulipia na sio free kama .com na zingine sio blogspot japo hili sio lazima sana lakini ukihitaji wakukubalie haraka nunua dommain, Habari ya domain age ni kwa nchi kama india ndio wanafuata sana ambapo wanaitaji iwe imetimia miezi 6
  • Age Verification 
Unatakiwa uwe na miaka kuanzia 18 na kuendelea ndipo ujiunge na kampuni hili
  • Traffic 
Website yako inatakiwa kuwa na pageviews 50per day ndipo wanaweza kakakubalia
  • Relevants pages
Google adsense wanaitaji website yako iwe na pages zifutazo zilizoandikwa vizuri na kwa ukweli wa hali ya juu kwa sababu wanazisoma Privacy policy, disclaimer, about Us and contact forms. Kwemye hizo page tafadhari kama utaweka email weka email uliyojisajilia google ili wajue kuwa ni mtu halali. mfano click here kuona mifano ya hizo pages na jinsi zilivoandikwa KAMA WEBSITE YAKO HAINA HIZI KAMWE HAIWEZI KUKUBALIWA
  • Poor navigation
Website yako inatakiwa imuwezeshe na kumrahishisia mtembeleaji kuona content zako bila usumbufu na epukakutumia rangi kwenye blog post tumia black and white
  • Youtube Momentization
Hakikisha unapost video kwenye website yako ambazo umemomentise kwenye channnel yako kama hujamomentise usipost kwa sababu hawatakukuballia kamwe jinsi ya kumomentise tutaanda makala yake.

MUHIMU:HAKIKISHA WEBSITE YAKO INAKUWA SAFI NA HAINA MARANGI YANYOONEKANA

MAKALA ZINAZOFUATA
  • jinsi ya kujiunga(hatua)
  • jinsi ya kumomentise youtube video
  • kupitia terms na policy baada ya kukubaliwa
  • jinsi ya kuweka adsense code(blogs,wordpress,durplar)
  • jinsi ya kudownload adsense blog templates supported
  • jinsi ya kujiunga na paypal ili kuweza kupokea malipo
  • jinsi ya kuchanganya adsense codes na za makampuni mengine
  • jinsi ya kuongeza mapato yako yaani tricks mbalimbali
  • n,k
KWA MAONI AU SWALI ULIZA KWENYE COMMENT BOX NA NTAKUJIBU KWA UFASAHA 

HAIRUHUSIWI KUCOPY MAKALA HII BILA RUHUSA 
Labels:

Post a Comment

Medson

{facebook#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {twitter#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {google-plus#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL}

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget