JE, GOOGLE PLAY STORE YAKO INASUMBUA? PATA UTATUZI HAPA!


Google Play Store
Google Play Store ni moja kati ya 'APPLICATION' za msingi kwa mtumiaji wa simu janja A.K.A  ''Smart Phones''.

>>> Kuna wakati 'Play Store' inakuwa inasumbua, ambapo mtumiaji 
anashindwa kufanya vitu mbalimbali kwenye simu yake kama

vile ku 'kudownload' applications, au pia kuzi 'update' na pia tatizo la kujifunga 'yenyewe' na kuleta ujumbe wa ''Unfortunately Google has stopped''

JINSI YA KUTATUA TATIZO HILI

1. Force close the Google Play Store
>>Hapa unailazimisha Play store ijifunge. Fanya hivi, nenda Setting > Apps > All halafu ichague Google Playstore halafu click Force stop. Hii inaweza ikamaliza tatizo lililojitokeza awali.



Picha; Force stop au Unistall

2. Zima mtandao kabisa yaani weka 'Airplane mode'
>>Hamna ufanisi sana kwenye njia hii kwa baadhi ya simu lakini hii njia huwa inachagua baadhi ya simu! Kwenye Tecno na Huawei inakubali sana!


                                    


3. Cheza na Wifi
>> Jaribu kuzima na kuwasha Wifi kwenye Android yako maana tatizo linaweza likawa ni mtandao wa simu yako.

4. Restart simu yako (Reboot)
>> Kulingana na mpangilio wako  wa simu, Restart simu yako ili ku clear cache ambayo pengine inaweza ikawa inasababisha tatizo hilo. Kwa Smart Phone nyingi, ku restart, bonyeza Power buttonkwa sekunde kama 7 halafu chagua Reboot au Restart kulingana na simu yako! Kwa wengine angalia mpangilio wa simu yako!


                                    


5. Futa Google Play Store cache au Data
>> Nenda Setting > Apps > All > Play Store, ichague, halafu click Clear/ Wipe cache na Data kulingana na simu yako!

6. Angalia kwenye 'Disabled Apps'
>> Huenda Play Store ilikuwa imeshitishwa kwenye simu yako, kwa hio lazima uiruhusu kuendelea kufanya kazi!KIVIPI SASA??? 
>> Nenda Setting >> Apps > All, halafu shuka mpaka chini ambapo Apps zilizokuwa Disabled hukaa, halafu ichague hio Play Store kama ipo hapo, halafu click Enable.


                                   


7. Uninstall Google Play Store
>> Fanya kwenda Setting > Apps > All> Play Store, ichague, halafu click  Unistall Updates.

8. Ondoa na ingiza Google Account yako
>> Nenda Setting > Accounts na chagua akaunti yako ya google!  Halafu gusa kwenye vidoti vitatu,na chagua Remove. Then jaribu kuiingiza Account yako tena kuangalia kama tatizo la Playstore limetatulika!

9. Factory data RESET
>>Baada ya njia zote hizi kufeli, hamna budi kui futa data zote na kuanza upya kabisa! JE, UNAJUA JINSI YA KU ''FACTORY RESET'' simu yako??? 


                                      

Somo linakuja mda si mrefu, kwa sasa Tembelea hapa kwa masomo yaliyopita!

>>> Je, wewe huwa unatumia njia ipi kutatua hili tatizo??? Weka comment hapo chini!!
Labels:

Post a Comment

Medson

{facebook#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {twitter#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {google-plus#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL}

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget