/pattern files kwenye Linux Operating System hii sitaizungumzia leo....
Onyo: Njia Hii Itafuta Kila Kitu Kwenye Simu Yako Na Kurudia Ilivyokuwa Mpya, Yaani bila Zile Application Ulizodownload Mwanzo..
Kwa Kutumia Njia Ya Kwanza Fanya Yafuatayo...
1. Hakikisha simu yako ina charge ya kutosha kama sio full kabisa.
2. Zima simu yako na utoe sim card yako(line) na memory card yako pia.
3. Bonyeza Kitufe cha kuongeza sauti kwenye simu huku ukibonyeza kitufe cha kuwashia simu, shikilia vyote kwa pamoja mpaka itakapo anza kuwaka.
Hii hutofautiana baina ya simu, kuna zingine unatakiwa kubonyeza kitufe cha home + kitufe cha kuwashia
4. Simu yako Itakupeleka sehemu itakayo kuwa na kama ifuatavyo katika picha
Kwa simu za Android ya kawaida utaota hivi
Kwa Simu zingine utaona hivi hapa chini
5. Sasa tumia vile vitufe vya sauti kupandisha au kushusha kuelekea chaguzi unayoihitaji.
6. Nenda kwenye wipe data/factory reset kisha bonyeza kitufe cha kuwashia
(Hapa Kitufe cha kuwashia kinatumika kwa kuchagua unachohitaji)
Kwa simu za kichina chagua ile chaguzi inayofanana na picha ya pili pale juu.
Kwa wataoona simu zao hazifanani na zile zilizopo juu tafadhari chagua factory reset unayoiona au wasiliana nasi kwa namba za simu zilizopo juu kabisa.
7. Baada ya hapo simu itafanya reset yenyewe . Ikishamaliza utaona imekuwa kama hivi hapa chini
8. Baada ya hapo chagua restart your phone kumbuka kutumia vitufe vya sauti kushusha au kupandisha na kitufe cha kuwashia kuchagua.
9. Simu yako itawaka bila kuuliza password,,,, Hongera Umefanikiwa
Post a Comment